Mwenyekiti
wa tume huru ya kimataifa ya kusaka ukweli nchini Myanmar, FFMM,
Marzuki Darusman amesema hayo alipozungumza na waandishi habari huko
Geneva, Uswisi, baada ya timu yake kukutana na Warohingya huko Cox Bazar
nchini Bangladesh ambako wamekimbilia kupata hifadhi na usalama wa roho
zao.
''Hali haijatengamaa Myanmar kikamilifu. Tunaendelea kusikia uchomaji moto ukiendelea. Hili linaendelea kuathiri jamii hii.''
Amesema
ukatili huo pia unajumuisha mauaji ya halaiki, ubakaji wa makundi na
watu kukamatwa kiholela na kuongeza kuwa: ''Ushahidi huo kwa hakika
utatumiwa kuandaa hitimisho na mapendekezo kwenye Baraza la Haki za
Binadamu, yatakayojumuisha hatua za kinidhamu kwa wahusika wakuu wa
ukatili huu wa halaiki."
Mwezi
Disemba mwaka jana, wajumbe watatu wa tume ya FFMM, walitembelea
Malaysia kwa siku tano na walikutana na jamii za wakimbizi wa jamii ya
Rohingya. Ripoti yao itawasilishwa mbele ya Baraza la Haki la Umoja wa
Mataifa mwezi Machi mwaka huu.
Kuanzia
Agosti 25 mwaka huu hadi hivi sasa, vikosi vya usalama vya Myanmar
vimechoma moto vijiji visivyopungua 350 katika eneo la Waislamu huko
Rakhine, magharibi mwa nchi hiyo.
Katika makubaliano yaliyofikiwa baina ya
Aung San Suu Kyi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Myanmar na Abul
Hassan Mahmud Ali, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Bangladesh, serikali
ya Myanmar iliahidi kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Kiislamu wa nchi
hiyo ambao filihali wanaishi katika mazingira magumu sana kwenye katika
mpaka wa nchi mbili hizo.
Jinai
za jeshi la Myanmar na Mabudha wa nchi hiyo dhidi ya Waislamu wa jamii
ya Rohingya zinaendelea katika hali ambayo, serikali ya nchi hiyo
iliahidi kuandaa mazingira ya kurejea makwao wakimbizi wa Kirohingya.
chanzo: parstoday.
Comments