
Akitangaza sehemu ya baraza lake jipya, Rais huyo wa Kenya pia amependekeza wanasiasa wawiwili kuchukua nafasi za uwaziri.
Kinachoshangaza
wadadisi wa maswala ya kisiasa ni kutangazwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka
wa Kenya, Bw KeriakoTobiko kuwa waziri. Hii ni mara tu baada ya Uhuru
Kenyatta kutangaza kwamba amekubali maombi ya Bwana Tobiko ya kujiuzulu
kama Mkurugenzi wa Mashtaka wa Kenya.
Waliohifadhiwa katika baraza
hilo jipya ni Waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiangi, Waziri wa fedha
Bwana Henry Rotich, Waziri wa Utalii Najib Balala, na Bwana Joseph
Mucheru akihifadhi wadhifa wake wa Waziri wa Teknolojia na Habari.
Waziri wa Mawasiliano amesalia kuwa Bwana James Macharia na Waziri wa
Kawi ni Bwana Charles Keter.
Wanasiasa walipoendekezwa na rais kushikilia wadhifa wa uwaziri
ni aliyekuwa Seneta wa Jimbo la Turkana ,John Munyes na aliyekuwa Govana
wa Marsabit , huko Mashariki mwa Kenya Bwana Ukur Yatani ,
Kiongozi
huyo wa Kenya anayehudumu kwa kipindi chake cha pili na cha mwisho kama
rais amesema bado yuko katika harakati ya kubuni baraza lake kamili .
Katiba ya Kenya inasema kwamba baraza la mawziri sharti liwe na mawaziri kati ya 14 na wasizidi 22.
Rais
Uhuru Kenyatta aliingia madarakani kuwa awamu wake pili baada ya
kutangazwa mshindi wa urais baada ya uchaguzi wa marudio nchini Kenya
mwezi Oktoba mwaka 2017.
chanzo:Bbc.
Comments