Tuhuma za uchochezi zamfikisha Sugu mahakamani.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo Januari 16, 2018 amefika katika mahakama kuu Kanda ya Mbeya pamoja na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wakituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi yenye kuleta chuki baina ya wananchi na serikali.

Hapo jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram aliandika; ‘polisi wameniita  wanipeleke mahakamani kwa wanachodai ni ‘Uchochezi’ najiskia kama Nyerere wakati wa Ukoloni au Mandela wakati wa Ukaburu, Siogopi na msiogope’.

Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Emmanuel Masonga wanadaiwa kutoa maneno yenye kuleta chuki baina ya wananchi na serikali katika mkutano walioufanya December 30 mwaka jana.

chanzo: zanzibar24.

Comments