
Ndani ya kitabu
hicho kilichoandikwa na mwandishi wa habari Michael Wolff,afisa huyo wa
zamani wa ikulu ya Marekani,ameelezea namna ambavyo Donald Trump
mtoto,mwanaye rais Trump alivyopewa taarifa na Urusi zilizolenga
kummaliza kisiasa Bi Hillary Clinton ili yeye aweze kushinda.
Hata
hivyo kutokana na shutuma hizo ndani ya kitabu hicho zilizopewa uzito
na afisa huyo wa zamani wa ikulu ya white house,rais Donald Trump
amesema kuwa lolote la kuweza kumuathiri yeye binafsi na urais wake
pia,bali amesisitiza kuwa amegundua kuwa ofisa huyo hakupoteza kazi yake
tu lakini alipoteza akili zake pia.
''Steve alikuwa ofisa aliyekuwa akifanya kazi kwaajili
yangu,mara baada ya mimi kuteuliwa kuwania urais baada ya kuwabwaga
wagombea wengine 17,'' amesema Trump.
Amesema pia kuwa Steve
anafanyayote hayo kwa maslahi binafsi,akifikiri kuwa suala la ushindi si
rahisi kama ilivyokuwa katika ushindi wangu,hana lolote la kuweza
kufanya kuhusiana na historia ya ushindi wetu ambao ulipatikana kwa kura
za wanawake na wanaume waliokuwa wamesahaulika.
Steve Bannon, ni
afisa wa zamani wa rais Trump nayetajwa kuwa mtu muhimu na alibuni kauli
mbiu ya rais Trump Marekani kwanza yaani America first kabla kuacha
kazi mwezi August mwaka jana.
chanzo:Bbc.
Comments