Klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini nayo imeingia katika vita ya kumtwaa mshambuliaji Elius Maguri.
Taarifa
za uhakika zinaeleza, Cape Town City imefanya mazungumzo na wakala wa
mchezaji huyo ambaye pia bado anawaniwa na Difaa Al Jadid ya Morocco
anayoicheza Saimon Msuva.
Awali
ilielezwa anaweza kujiunga na timu nyingine ya Afrika Kusini lakini
sasa Cape Town City ambayo inajiimarisha inaonyesha nayo imeingia katika
mbio hizo.
Mazungumzo kati ya wakala wa Maguri na Difaa yanaonekana kwenda vizuri na kama yatakaa sawa, anaweza kujiunga nayo.
“Kweli kumekuwa na mazungumzo na yanakwenda vizuri sana. Hapo limebaki suala la maslahi,” kilieleza chanzo.
Comments