
Akizungumza na Waandishi wa Habari baaada ya kutiliana saini na Balozi mdogo wa China Nchini Tanzania , Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Khalid Salum amesema Zanzibar imekuwa ikinufaika na ruzuku hiyo kwa muda mrefu ambapo kwa sasa kiwango cha ruzuku hizo kimeongezeka.
Amesema awali Serikali ya Zanzibar ilikuwa ikinufaika na Ruzuku hiyo kwa kutoka shilling milioni 20 za kichina hadi kufikia milioni 100 jambo ambalo linaimarisha Mashirikiano kati ya nchi mbili hizo.
Akizungumzia matumizi ya Fedha hizo Dk,Khalid amesema ruzuku hiyo inakusudiwa kwa mahitaji mbali mbali ikiwemo kutumika katika ujenzi wa taa za barabarani kuanzia Malindi-Bububu na Mkapa Road- Amani .
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania aliepo Zanzibar Vie Xiao Wu amesema Serikali ya China itaendelea kushirikiana na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Miradi ya maendeleo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya .
chanzo:zanzibar24.
Comments