Singida yafuzu hatua ya nusu fainal Kombe la Mapinduzi.

KIKOSI cha Singida United kimefudhu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Mlandege ya Unguja mabao 3-0.
Singida ambayo imepangwa kundi B pamoja na timu za Yanga ya Tanzania Bara, Mlandege, JKU, Taifa Jang'ombe na Zimamoto za Zanzibar, imefudhu baada ya kushinda mechi tatu na kufikisha pointi tisa.
Iliifunga Zimamoto 3-2, Taifa Jang'ombe 3-1 na mchana wa leo, imeifunga Mlandege ambapo sasa inaisubiri timu moja kati yahizo kwenda nayo nusu fainali.
Singida iliyocheza mechi tatu mfululizo tangu ilipowasili Kisiwani Zanzibar, itarudi uwanjani kesho Jumamosi kukipiga na JKU ya Unguja.

Comments