
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO, Masanja Kadogosa ameithibitishia
Idara ya Habari (MAELEZO) kuanza kwa mchakato huo ambao unafuata
taratibu za kimataifa za ununuzi kwa njia ya ushindani.
Kwa mujibu wa tangazo la zabuni, jumla ya vichwa 14 vya treni ya
umeme kwa ajili ya kusafirisha mizigo na vichwa viwili vya treni ya
mizigo inayotumia mafuta vinahitajika.
Aidha, RAHCO pia imetoa zabuni ya ununuzi wa vichwa vitano vya treni
ya abiria ya kisasa inayotumia umeme (Electric Multiple Units) ambapo
kila kimoja kitakuwa na uwezo wa kuvuta mabehewa 60 yenye kuchukua
abiria 1,800.
Katika mabehewa hayo ya abiria, mabehewa 15 yatakuwa ni ya kiwango cha daraja la kwanza na mengine 45 ni daraja la pili.
Mbali na mabehewa ya abiria, zabuni hiyo inajumuisha ununuzi wa
mabehewa mengine zaidi ya 1,500 yenye muundo tofauti kwa ajili ya
kubebea aina mbalimbali za mizigo.
Pamoja na sifa mbalimbali zilizo ainishwa katika tangazo la zabuni,
moja ya sifa za reli hiyo ya kisasa ni kuhimili treni ya abiria yenye
uwezo wa mwendo kasi wa kilometa 160 na mabehewa yenye juma ya urefu wa
mita 2000, wakati ile ya mizigo yenye uwezo wa kwenda kasi ya kilometa
120 kwa saa.
Kwa mujibu wa tangazo la zabuni, mwisho wa kuwasilisha nyaraka za
zabuni ni Januari 30, mwaka huu.Tayari awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli
hii kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro inaendelea na wakati huo huo
tayari Serikali imesaini mkataba kwa ajili ya awamu ya pili ya ujenzi
kutoka Morogoro hadi Makutupola mkoani Dodoma.
chanzo:Zanzibar24
Comments