Gazeti la Times of India limeandika
kuwa, idadi ya vijana wanaojiua imezidi kuongezeka kiasi cha kuwafanya
viongozi wa serikali ya nchi hiyo kuanza kuzitahadharisha familia.
Kwa
mujibu wa takwimu za mwisho zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
India kuhusiana na suala hilo, sababu ya vijana wengi kujiua ni utumiaji
wa madawa ya kulevya, matatizo ya kisaikolojia yanayosababishwa na
kuachana wazazi wawili, kugombana na watu wakubwa, masuala nyeti na
matatizo yanayohusiana na masomo.
Weledi wa
mambo nchini humo wanaamini kwamba, mabadiliko ya haraka katika jamii ya
India yamekuwa na taathira hasi kwa vijana wa nchi hiyo ambapo kutokana
na kutokuwa na uwezo wa kufanya mawasiliano chanya na watu wa familia
na marafiki zao, huamua kujiua.
Hii ni katika hali ambayo India pia
inaongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha vijana wanaojiua duniani.
Weledi wa mambo wanaamini kwamba kabla ya serikali kutatua tatizo la
kisaikolojia kwa vijana, inatakiwa kwanza kushughulikia hali ya uchumi
na kutatua matatizo ya kijamii nchini humo.
Comments