"Nimepokea
kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kutokea kwa ajali
iliyosababisha ndugu zetu takribani 36 kupoteza maisha baada ya basi la
abiria kugongana na roli katika barabara ya Nakuru - Eldoret nchini
Kenya.
Msiba
huu umesababisha majonzi makubwa sio tu kwa ndugu zetu wa Kenya bali
pia kwetu sote wana Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumepoteza wapendwa
wetu na nguvu kazi yetu.
Kwa
niaba ya Watanzania wote nakupa pole sana ndugu yangu Mhe. Uhuru
Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa msiba huu mkubwa ulioupata,
nawapa pole wana familia wote waliowapoteza jamaa zao na pia nawapa pole
wananchi wote wa Kenya.
Naungana
nanyi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, nawaombea majeruhi wote
wa ajali hii wapone haraka na Marehemu wote wapumzishwe mahali pema
peponi, Amina".
Hizi
ni salamu za rambirambi alizozitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe.
Uhuru Kenyatta kufuatia ajali ya barabarani iliyosababisha vifo vya
watu takribani 36 baada ya basi la abiria kugongana na roli katika
barabara ya Nakuru - Eldoret nchini humo tarehe 31 Desemba, 2017.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
31 Desemba, 2017
chanzo:mpekuziblog.
Comments