
Tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya Shangani Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Hassan Nassir Ali, akizungumza na
Nipashe kisiwani hapa jana, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa
9:30 usiku baada ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2018 akiwa na marafiki
zake hao.
Alisema kabla ya kukutwa na umauti, Winkdl akiwa na marafiki zake
wanne ambao wanadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, waligombana na
baadaye ugomvi huo kusababisha kuchomwa kisu katika sehemu mbalimbali
za mwili wake.
Kamanda Ali alisema watuhumiwa hao wanne ambao wote ni wanawake, raia
wa Tanzania na Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikilia kwa ajili ya
kuwahoji na kukamilisha taratibu za kiuchunguzi.
“Inasemekana wote walikuwa wameshalewa na inadaiwa kuwa
chanzo cha ugomvi ni wivu wa kimapenzi, lakini tunaendelea na
uchunguzi,” Kamanda huyo alisema.
Aidha, Kamanda Ali alibainisha kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mnazimmoja kisiwani hapa.
Aliongeza kuwa raia huyo wa kigeni alikuwa anaishi Zanzibar akiwa ni
msimamizi wa mapishi katika hoteli moja ya kitalii kisiwani hapa.
chanzo: zanzibar24.
Comments