Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametishia kung’oa
kiongozi mkubwa wa Chadema ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
Ameyasema
hayo mara baada ya madiwani wawili wa CHADEMA kuachia ngazi Mjini
Iringa, ambapo amesema kuwa hoja za madiwani hao wanakimbia ubabe wa
mchungaji Msigwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo.
"Leo
Madiwani wengine wawili wamehama na kujiunga na CCM. Ukiwasikiliza
kilichowaondoa ni Uongozi Mbovu na Ubabe pale Iringa Mjini. Nasikia
wameambiwa "never outshine your master". Mimi nilidhani "masta" ni
wananchi kumbe ni "pasta". Ukitukana tusi moja Kiongozi mmoja nachomoa
DSM " Ameandika Polepole
Siku
za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la viongozi wa kisiasa ndani ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kuhamia chama tawala cha
CCM.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments