Majimaji inayoendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Majimaji Songea chini ya kocha Mkuu, Peter Mhina imepoteza mechi hizo ambapo mchezo wa 11 ilikutana na Ruvu Shooting na kuchapwa mabao 2-1, pia Disemba 30 mwaka jana ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Wachezaji walikosekana kwa mechi hzio ni Selemani Selembe, Paul Mahona, Tumba Sued pamoja na Abdallah Salamba ambao hawakuwepo katika kikosi hicho kutokana na matatizo mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa Ofisa habari wao, Onesmo Ndunguru ilisema tayari wachezaji watatu wamesharejea na kujiunga na wachezaji wenzao kwenye mazoezi isipokuwa Abdallah Salamba bado yupo kwao.
“Salamba hajarejea hadi sasa na aliondoka hapa kwa ruhusa maalumu kutokana na kupata taarifa kwamba nyumbani kwao kuna matatizo ya kifamilia, lakini yote kwa yote anaweza akarejea hata ndani ya wiki ijayo,”
Aliongeza, “Ni imani yetu kwamba kurejea kwa wachezaji hao kutakipa kikosi nguvu ya kufanya vizuri kwenye mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho (FA) pamoja na mechi mbili zilizo mbele yetu tutakazocheza Uwanja wa nyumbani,” alisema Ndunguru.
Alisema wanaiona michezo hiyo kuwa migumu kwao kwani timu wanazokutana nazo siyo lelemama na huwa hazifungwi kizembe, kwa hiyo wasipojipanga vyema wanaweza kuwa katika hali mbaya zaidi kutokana na pointi 11 walizonazo kwa mechi 12.
Comments