Taarifa ya Idara ya Sheria ya Marekani imesema kuwa, hukumu dhidi ya Daniel Pye mwenye umri wa miaka 36 ilitolewa jana Jumatano.
Mmishonari huyo alipatikana na hatia mwezi Novemba mwaka jana, ambapo alikuwa anakabiliwa na mashitaka matatu, likiwemo la kusafiri katika nchi ya kigeni kwa lengo la kushiriki ngono na watoto wadogo.
Pye anaripotiwa kuwanajisi mabinti waliokuwa katika kituo cha mayatima alichokuwa akisisimamia katika mji wa Jacmel nchini Haiti, kati ya mwaka 2006 na 2012.
Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Marekani, takriban makasisi 6,900 wa Kanisa la Katoliki la Roma wanadaiwa kuwalawiti watoto wadogo 16,900 kati ya mwaka 1950 na 2011.
chanzo:parstoday
Comments