Mbaroni kwa kumchoma moto mtoto wa kaka yake.

Jeshi la polisi Mkoa wa Mara  linamshikilia Nyandaro Kusoya mkazi wa kijiji cha Nyang’oma kwa tuhuma za kumchoma moto mikono yote miwili mtoto wa kaka yake, Sarah Kaela.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa  Polisi  Mkoa wa Mara Jaffary Mohamed, amesema mtuhumiwa huyo Nyandaro Kusoya mwenye umri wa miaka 29 alimchoma moto mtoto huyo wa kaka yake, Sarah Kaela mwenye umri wa miaka mitatu kwa kile kinachodaiwa alifanya  kosa la kulamba sukari.

Bibi wa mtoto huyo Nyamata Chihoye amesema mtuhumiwa huyo Nyandaro Kusoya alimfata mjukuu wake huyo  na kuondoka naye kwa lengo la kwenda kuishi naye katika kijiji cha Nyang’oma Musoma vijijini Mkoani Mara na matokeo yake kusikia mjukuu wake amefanyiwa kitendo cha kikatili.

Aidha Kamanda Mohamed amesema wanafanya taratibu za kisheria ili kuhakikisha wanamfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Chanzo: zanzibar24.

Comments