Kocha
Mkuu wa Mbao FC, Ettiene Ndayiragije raia wa Burundi, amewasifu vijana
wake kutokana na kufuata maelekezo yaliyowafanya kuibuka na ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Yanga, wikiendi iliyopita.
Katika
kuwasifu huko, ameahidi kuendelea kuifunga timu hiyo kila atakapokutana
nayo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, uliopo jijini Mwanza.
Ikumbukwe
kuwa, Jumapili iliyopita, Mbao iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi
ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza.
Hii
ni mara ya tatu kwa Yanga kufungwa na Mbao uwanjani hapo, kwani msimu
uliopita katika mechi ya ligi kuu, Mbao iliifunga Yanga bao 1-0, kisha
ikaibuka tena na ushindi kama huo katika Kombe la FA.
Miaka ya nyuma,
Yanga ilikuwa na matokeo mazuri uwanjani hapo lakini si dhidi ya Mbao,
bali ilipokuwa ikipambana na Toto Africans.
“Siri
ya sisi kuwa bora dhidi ya Yanga nadhani ni namna ambavyo vijana
wamekuwa wakifuata kile ambacho nimekuwa nikiwaelekeza, si tunapocheza
na Yanga tu, bali hata na timu zingine hasa kwenye uwanja wetu wa
nyumbani tumekuwa tukifanya vizuri sana.
“Hatutaki
kuona tunapoteza mechi hapa kwetu ndiyo maana tumekuwa tukijitahidi
sana kucheza kwa juhudi, hata Simba inapokuja huku inapata shida
kuondoka na pointi.
“Kama
wakiendelea kutudharau kila wakija huku na kujiaminisha kwamba lazima
washinde, basi tutakuwa tunawafunga kila siku,” alisema Ndayiragije.
Comments