
Kuanzia
sasa Januari mosi mwaka 2018 watu walio na umri wa kuanzia miaka 21,
wanaweza kumiliki hadi gramu 28 za bangi na kupanda hadi miti 6 ya bangi
nyumbani.
Wanaopinga wanasema kuwa sheria hiyo itasababisha watu
kuendesha magari wakiwa tayari wamevuta bangi kuchangia vijana kuvuta
bangi.
Lakini biashara zinatabiri kile kinaonekana kuwa sekta ya mabilioni ya dola miaka michache inayokuja.
Wakaazi
wa Califonria walipigaa kura kuunga mkono kipengee cha kuhalalisha
bangi miaka 14 iliyopita katika kura ambayo ilifanyika sambamba na
uchaguzi wa rais nchini humo.
Tangu wakati huo sheria ngumu zinazohusu kodi zimeandikwa kudhibiti mauzo ya bangi.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ambayo inafuatilia soko la bangi duniani
alitabiri kuwa kutakuwa na kushuka kwa bei kwa mwaka wa kwanza au miaka
miwili.
Hata hivyo, faida ni kubwa katika jimbo hilo tajiri zaidi na lenye watu wengi zaidi nchini Marekani.
Mwaka 1996, California lilikuw jimbo la kwanza kuhalalisha bangi kwa matumizi ya matibabu.
Inakadiriwa
kuwa soko la bangi haramu kwa sasa ni dola milioni 5.1 na wakati
itahalalishwa thamani yake itakuwa ya dola bilioni 5.8 itakapofikia
mwaka 2021.

chanzo:Bbc.
Comments