Dar es Salaam. Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imewapeleka kwenye kamati ya maadili viongozi wanne wa soka kwa kosa la udanganyifu na kughushi.
Viongozi hao ni Msimamizi wa kituo cha Mtwara, Dunstan Mkundi, Katibu wa Chama cha Soka Mtwara, Kizito Mbano,Mhasibu msaidizi wa Simba, Suleiman Kahumbu na Katibu msaidizi wa Ndanda , Seleman Kachele.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na TFF kwenda kwa vyombo vya habari imesema kuwa Sekretarieti inawashtaki viongozi hao kwa makosa ya kughushi pamoja na udanganyifu wa mapato katika mchezo namba 94 kati ya Ndanda na Simba uliofanyika Desemba 30 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara.
Viongozi hao wametakiwa kufika mbele ya Kamati ya Maadili, Alhamis.
Kamati hiyo ya maadili inaongozwa na Mwenyekiti, Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu mwenyekiti wakili Sreven Zangira wakati wajumbe ni Glorious Luoga, Walter.
Comments