Akizungumza katika kikao cha wazee pamoja na mashekhe wa mji wa Tumbe
Sheha wa Shehia ya Tumbe Mashariki Nd. Seif Omar Khamis amesem kwa sasa maadili
yamepotea hivyo ipo haja jamii kuungana ili yasizidi kudidimia.
Amesema bilaya mashirikiano ya pamoja hakuna jambo lolote ambalo
litaloleta matunda na mwisho wake nikuzaa kizazi kilicho kosa maadili mema.
amefahamisha kuwa kukithiri kwa wizi ma mazao, mifugo na hata
vitendo vya udhalilishaji vimechangiwa kwa asilimia kubwa na ukosefu wa maadili
ndani ya jamii.
Aidha ameitaka jamii ya watu wa Tumbe kupitia mashekhe kuendelea
kuelimishana juu ya vitendo vya udhalilishaji ikiwemo liwati kwani vitendo
hivyo vinaikosesha hadhi na heshma jamii
yao.
Kwaupande wake Sheha wa Sheia ya Tumbe Magharibi Nd. Masoud Khamis
amesema Tumbe imejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo Mmikorosho na Mikoko
hivyo nivyema kuzitumilia ipasavyo bila kuathiri mazingira hatimae kusababisha
majangwa.
Akizungumzia kuhusu wizi wa mifugo Sheha huyo amesema kwa sasa
wanajiandaa kuunda sheria ndogo ndogo zitakazo wasaidia kupambana na wale wote
watakao jari kufanya vitendo hivyo.
Nae mmoja ya waulamaa wa mji wa Tumbe Utasdh Juma Abdurrahman Juma
aesema lazima jamii ijuwe kuwa Allah ( SW ) ametuleta duniani kwa ajili ya
kumuabudu nasivyenginevyo hivyo nivyema kurejea kwake pale tulipo kosea ili
aweze kutusamehe.
Comments