
Akizungumza na Zanzibar24 Katibu wa
Mahakama ya Vileo Saleh Ali Abdalla amesema licha ya mahakama
kujiridhisha vya kutosha katika ukaguzi wa baa zinazofanya biashara hiyo
Zanzibar na kuridhia kuwapa vibali baadhi ya wafanyabiashara lakini
endapo kutatokea uvunjifu wa sheria kwa waendesha biashara hiyo mkono wa
sheria utawaadhibu.
Amesema kupewa kibali cha kuuzia biashara
ya pombe wamiliki wa baa sio mwanya wa kuwaudhi wananchi kwa kuwafanyia
fujo za miziki na kuuza biashara hiyo kiholela kwa watoto chini ya umri.
Mahakama imesema itaendelea kufuatilia
Mwenendo wa biashara hizo ili kuondoa malalamiko kwa wananchi na
kufuatilia kwa ukaribu mapato ya Serikali yatokanayo na biashara hiyo.
chanzo:Zanzibar24.
Comments