
Wazima
moto walisema kuwa moto huo katika jengo la King's Dock karibu na
ukumbi wa Liverpool Echo Arena, ni mioto mibaya zaidi kuwai kukabiliana
nayo.
Polisi walisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa moto kutoka kwa gari ulisambaa kwenda kwa mengine.
Watu walihamishwa kutoka majengo yalito karibu kutokana na moshi.

Polisi
wa Merseyside walisema kuwa magari ya kuzima moto 21 yalikuwa eneo
hilo na huma za wazima moto zilesema zilikuwa zinachukua tahadhari ya
jengo hilo kuporomoka.
Magari yote yaliyokuwa kwenye jengo hilo linaloweza kuegeshwa magari 1600 yaliharibiwa. kwa mujibu wa polisi.
Waliwashauri watu kubaki manyumbani mwao na kufunga madirisha ikiwa wangeona moshi kutoka kwa moto huo.

chanzo;Bbc.
Comments