Mtaalamu
wa Uchumi, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuna haja ya kuwa na mjadala
wa kitaifa kuhusu uchumi na mustakabali wa Taifa.
Profesa
Lipumba ameyasema hayo jana Jumapili Desemba 31,2017 wakati wa
mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam kujadili hali ya uchumi kwa
mwaka 2017.
Alisema
kuna haja ya kujadili sera za kiuchumi, namna ya kujenga uchumi
unaoongeza ajira kwa wananchi na kutafuta suluhisho la matatizo
yanayowakabili Watanzania.
“Tuitishe
mjadala wa kitaifa tuje kujadili, tutazame upya sera za kiuchumi, namna
ya kujenga uchumi unaoongeza ajira utakaoleta manufaa kwa wananchi
wote. Tujadili kimsingi na tutoke na sera ambazo tunaweza kuishauri
Serikali nini cha kufanya,” alisema Profesa Lipumba.
Katika
mjadala huo, Profesa Lipumba alisema Serikali haiwezi kufanikisha
mapinduzi ya viwanda kama haijafanikisha ya kilimo kwa sababu ukuaji wa
kilimo ndiyo ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi.
Alisema
robo tatu ya Watanzania wanategemea kilimo lakini ukuaji wa sekta hiyo
ni mdogo kutokana na Serikali kukiacha nyuma kilimo na kukumbatia sekta
nyingine.
Profesa
Lipumba alisema kuna changamoto kubwa kwenye kilimo ambazo zinatokana
na ukweli kwamba, Serikali haijawekeza vya kutosha kwenye utafiti wa
kilimo, mafunzo kwa wakulima na usambazaji wa pembejeo.
“Tujifunze
kwa nchi za Asia kama vile China, India na Malaysia, wao wamewekeza kwa
wakulima wadogowadogo,” alisema Profesa Lipumba.
Mbunge
wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyeshiriki mjadala huo, alisema mfumo
wa elimu wa sasa wa Tanzania unamwandaa mtu kuwa tegemezi badala ya
kujitegemea kama ilivyokuwa zamani.
Alisema
kuna umuhimu wa kufumuliwa upya kwa mfumo huo tegemezi ili kujenga
utakaowafanya vijana wajifunze kujitegemea au ujasiriamali.
Bashe alisema Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa idadi kubwa ya mifugo lakini hakuna dira ya wazi ni wapi pajengwe viwanda.
Akichangia
mada ya hali ya uchumi, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha
Kampala (KIU), Dk Bravious Kahyoza alisema Tanzania haijazalisha ajira
za kutosha kwa wananchi kwa sababu ya kusinyaa kwa uchumi.
Alisema
Serikali imekuwa ikishindana kukopa na sekta binafsi jambo
lililosababisha sekta binafsi kubaki nyuma na kushindwa kuajiri watu
wengi kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi.
lietaka kuwepo uwiano kati ya sera za kifedha na zile za kibajeti ili kuleta matokeo mazuri kwenye uchumi.
“Wataalamu
wetu wanapaswa kukaa chini na kuangalia kama tuko kwenye njia sahihi
kuelekea mpango wa maendeleo wa miaka mitano na uchumi wa viwanda
ifikapo mwaka 2025. Kama hatuko sahihi basi ni vyema tukabadilisha mbinu
tunazotumia kufika huko,” alisema.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments