
Akizungumza na waandishi wa habari huko
katika ukumbi wa taasisis ya nyaraka na
kumbu kumbu za Serekali chake chake ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 54
ya Mapinduzi Zanizbar amesema azma ya serekali ni kuwafikishia wananchi wake
huduma ya umeme hadi vijijini na sasa lengo hilo naendelea kutekelezwa.
Amesema kwa kutimiza ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mh. Ali Mohd Shein alitoa kwawananchi wa kisiwa cha
fundo kupatiwa umeme sasa imekamilika.
amefahamisha kuwa
serekali ya Mapinduzi Zanzibar imefanya jitihada kubwa ya kupeleka umeme fundo
kwa kupitia wataalamu wa ndani na wamefanikiwa kulaza waya chini ya bahari
wewenye kiwango cha WALT. 1.7 kwa urefu wa km 2.4.
Amefafanua kuwa azma ya serekali ni kuwafikishia wananchi wa
visiwa vya unguja na pemba huduma ya umeme kwa haraka zaidi.
Jumla ya wananchi 352 wa kisiwa cha fundo wameshaunganishiwa huduma hiyo kati ya
wakaazi elfu 3000 waishio kisiwani humo.
Comments