
Alisema kuwa mapenzi yao hayataendelea akiwa na wajibu kama kiongozi wa chama lakini hana nia ya kujiuzulu.
Jo
Marney alikuwa ametuma ujumbe wa simu kuwa watu weusi wana sura mbaya
na mpenzi wake Prince Harry ataichafua familia ya kifalme.
Bw Bolton alisema kuwa ilikuwa kinyume na katiba ya chama cha UKIP kuonyesha fikra zozote za ubaguzi wa rangi.
Mwanajeshi huyo wa zamani alichukua usukani wa chama cha UKIP kama
kiongozi mwezi Septemba, na kuwa kiongozi wa nne katika kipindi cha
miaka 18.
Bw
Bolton 54, alisema kuwa mwanamitindo huyo wa miaka miaka 25 alitimuliwa
chamani mara moja baada ya chama kugundua kuhusu maoni yake.
Ujumbe huo ulitumwa wiki tatu baada ya wapenzi hao wawili kuanza uhusiano wao.

chanzo:Bbc.
Comments