
Katika
hotuba ya mwaka mpya iliyopeperushwa kwa njia ya runinga, alisema kuwa
Marekani inaweza kufikiwa na silaha za nyuklia za Korea Kaskania
akiongeza kuwa huo ni kweli na wala sio vitisho.
Lakini pia alitoa wito kwa Korea Kusini kuja kwenye mazungumzo.
Korea Kaskazini pia itatuma kikosi katika mashindano ya olimpiki ya msikmu wa baridi nchini Korea Kusini, Kim alisema.
Wakati aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu vitisho vya Kim, Rais wa Marekani alisema, "tutaona, tutaona".
Alikuwa akizungumza kando mwa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya katika eneo lake ya kifahari la Mar-a-Lago huko Florida.
Korea Kaskazini imewekewa vikwazo zaidi mwaka uliopita kwa
kutokana na mipango yake ya silaha za nyuklia na majaribio ya mara kwa
mara ya silaha hizo.
Taifa hilo lililotemgwa lilifanya majaribio 6 ya nyuklia ya chini ya ardhi na kuonyesha kuongeza uwo wake wa makombora.
Mwezi
Novemba ilifanyia majaribio kombora lake la Hwasong-15 ambalo lilipaa
umbali wa kilomita 4,475 mara kumi zaidi kuliko kituo cha safari za anga
za juu.
chanzo:Bbc.
Comments