Kamusoko, Ninja njia panda kuivaa Mwadui.

 Dar es Salaam. Nyota wa Yanga, Thaban Kamusoko, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Obrey Chirwa, Beno Kakolanya na Godfrey Mwashiuya wataikosa mechi ya leo Jumatano dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mazoezi ya Yanga yaliyofanya Jumatatu kwenye Uwanja wa Uhuru, kocha wa  George Lwandamina aliwapa wachezaji hao mazoezi yapekekayao.
Ilipofika wakati wa mazoezi ya kucheza mechi wachezaji hao walikaa benchi mpaka wenzao walipomaliza. Kamusoko, Mwashiuya na Ninja wanasumbuliwa na majeraha, wakati Chirwa anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu kwa kosa la kumpiga mcheza wa Prisons.
Lakini Kakolanya yeye alikuwa nje ya uwanja kutokana na kuidai klabu hiyo pesa yake ya usajili.
Hata hivyo, kocha Lwandamina alionekana kukitumia kikosi cha kwanza anachotegemea kukianzia kesho ni pamoja na kipa Rostand, Yondan, Tshishimbi, Andrew Vincent "Dante ', Emmanuel Martin, Ibrahimu Ajib, Radhamani Kessy, Juma Mahadhi, Said Juma Makapu, Haji Mwinyi na Buswita.
Wakati wachezaji waliokuwa wamevaa bipsi wakitumika kama wa akiba ni kipa Kabwili, Juma Abdul, Pato Ngonyani, Maka Edward, Gadiel Michael, Yohana Nkomola, Raphael Daudi, Amiss Tambwe, Matthew Anthony na Said Mussa.

Comments