
Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dar es salam katika ofisi za
makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania ambapo IGP Sirro amesema,
mkataba huo wa mashirikiano ya ulinzi utasaidia kutunza na kudumisha
amani kutokana na mashirikiano hayo.
Aidha IGP Sirro ameongelea mapigano ya majambazi ambao walikuwa
wakipambana nao kibiti walikimbilia msumbiji na muungano huo utaleta
mafanikio na kuwataka wote ambao wapo nchi msumbiji kuwa popote watakapo
kimbilia bado hawatakuwa salama.
Kwa upande wake IGP Bernadino Rafael wa Msumbiji amesema makubaliano
hayo yatawasaidia kuimarisha ulinzi na kubadilishana na kujifunza mbinu
mbalimbali ambazo jeshi la polisi la Tanzania wamekua wakizitumia ili
kudhibiti uhalifu na pia izi utazidi kuwa imara, na madhaifu madhaifu
ya polisi wa Tanzania.
chanzo: zanzibar24.
Comments