
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Simon Haule amesema tukio hilo limetokea Januari 1,2018
saa 9:45 alasiri.
Amesema Joseph Dogani alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa
risasi na polisi baada ya marehemu kutaka kuwapiga risasi askari
waliokuwa wanamfuatilia.
“Mtuhumiwa alikuwa akijihusisha na matukio mbalimbali ya
mauaji,unyang’anyi wa kutumia silaha na uvunjaji ,alikuwa anatafutwa
kuhusiana na tukio la kujeruhi na kumpora mlinzi silaha aina ya shortgun
iliyopatikana baada ya kuuawa kwa jambazi mwenzake”,ameeleza Kamanda Haule.
Kamanda Haule amesema baada ya kupekuliwa alikuwa akiwa na bastola yenye risasi nne ndani ya magazine.
chanzo: zanzibar24.
Comments