Kama unavyojua, tayari ratiba ya Kombe la Shirikisho Tanzania
bara (Azam Sports Federation Cup) rfaundi ya tatu tayari imeshatoka
baada ya draw kuchezeshwa leo January 5, 2018.
Story kubwa ni kuhusu mtanange kati ya Green Rangers dhidi ya Singida
United, hii inatokana na Warriors kuwatoa Simba mabingwa wa kombe hilo
msimu uliopita. Simba walijikuta wakitupwa nje ya mashindano katika
hatua ya pili ya mashindano hayo kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya
kutoka sare ya kufungana 1-1.
ShaffihDauda.co.tz imepiga story na Mkurugenzi wa Singida United
Festo Sanga kutaka kujua wamepokeaje ratiba hiyo inayowakutanisha na
wababe wa Simba katika raundi ya tatu ya ASFC.
“Sisi hatuwaogopi wala hatuwahofii hao Green Warriors tena tumepokea
ratiba kwa kufara kabisa kwa sababu tunajiamini kutokana na kikosi chetu
hata tungepangwa na Azam wala Yanga tungecheza nao tu”-Festo Sanga,
Mkurugenzi Singida United.
“Tutajiandaa kwa mchezo huo ambao tutacheza tukiwa ugenini nadhani
itakuwa uwanja wa Azam Complex, uwanja huo ni mzuri na unaruhusu mpira
kuchezeka.”
“Tumeingia kwenye kila kila mashindano kwa ajili ya kupambana
kuchukua ubingwa, hatupo kwa ajili ya kushiriki, kocha wetu Hans van
Pluijm anajua na wachezaji wanajua kwa hiyo tunataka kuchukua pia
ubingwa wa kombe FA.”
“Green Warriors kuwatoa Simba kwenye mashindano haimaanishi kwamba ni
wakali, isipokuwa ni matokeo ya mchezo wa soka. Kimsingi Simba ni timu
kama ilivyotimu zingine na inafungika kwa hiyo kutolewa na Warriors ni
sehemu ya soka.”
Ratiba kamili ya ASFC raundi ya tatu baada ya kuchezeshwa draw January 5, 2018.
Comments