![]() |
CLIFFORD NDIMBO WA TFF |
Kwanza
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kumpongeza
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe kwa
ufuatiliaji wake wa karibu wa michezo ikiwemo Mpira wa Miguu.
Baada
ya mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Dodoma FC vs Alliance na
Biashara vs Pamba kuliibuka malalamiko mengi ambayo yaliwafikia viongozi
wakuu wa TFF na kuyatolea tamko.
Taarifa
iliyotolewa na Mmoja wa maofisa wa TFF, Clifford Ndimbo imeeleza kuwa
Rais wa TFF, Wallace Karia alimuagiza Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Ndugu
Kidao Wilfred kufuatilia kwa kina jambo hilo ambapo hatua alizochukuwa
Kaimu Katibu Mkuu ni pamoja na kuwasiliana na Kamishna wa mchezo na
msimamizi wa Kituo cha Dodoma ambao wote walimpatia maelezo ya
kilichotokea na baada ya hapo Kaimu Katibu Mkuu akawasiliana na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi chombo kilichopewa dhamana ya kusimamia
Ligi zote kubwa nchini ikiwemo Ligi Daraja la Kwanza, Afisa Mtendaji
Mkuu naye alieleza Taarifa aliyopewa na Afisa wa Bodi aliyekuwa Dodoma.
Kaimu
Katibu Mkuu baada ya kuwasiliana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi
alikuwa na mawasiliano yaliyochukuwa muda mrefu na Katibu Mkuu wa
Baraza la Michezo Ndugu Mohamed Kiganja ili kupata taarifa kutoka vyanzo
mbalimbali kujiridhisha na jambo lililojitokeza.
Aidha
Kaimu Katibu Mkuu amekuwa na mawasiliano na Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Michezo nchini Yusuph Singo kuhusiana na suala hilo mara baada ya
michezo ile kumalizika na wamekuwa na ushirikiano mkubwa katika
kulifuatilia jambo hilo kwa karibu.
Baada
ya kupata taarifa mbalimbali Kaimu Katibu Mkuu alipeleka taarifa kwa
Rais wa TFF ambaye aliagiza Kikao cha Kamati ya saa 72 kikae haraka
iwezekanavyo ambapo Bodi ya Ligi walikuwa wanasubiri ripoti ambayo kwa
mujibu wa kanuni za Ligi ni saa 48 na tayari taarifa zote zimefika jana
kikao kimepangwa kufanyika kesho.
Rais
Karia bado aliona haitoshi hata kabla Waziri Mwakyembe "hajazungumza na
Waandishi wa Habari" aliita Wana Habari na kati ya alivyozungumza ni
kuhusu kinachoendelea Ligi Daraja la Kwanza na alionesha dhamira ya
kuwashughulikia wote wanaotaka kuharibu Ligi zetu kwa Upana wake na kwa
Ligi zote VPL, FDL na SDL na hasa kwa michezo inayohusisha timu za
Makundi yote zilizo katika nafasi ya kupanda au kushuka Daraja (FDL na
SDL) kuanzia mechi zinazolalamikiwa na kuhakiki za aina hiyo
zisizolalamikiwa,lakini pia katoa maagizo kwa Kaimu Katibu Mkuu
kuwaandikia barua TAKUKURU ili wachunguze matukio yote hayo
yaliyojitokeza na yanayoendelea na TFF ipo tayari kutoa Ushirikiano wa
kutosha katika Uchunguzi huo.
TFF
inapenda kusisitiza kuwa viongozi wake wakuu hawajihusishi na jambo
lolote lile la kupendelea mikoa wanayotoka ndiyo maana wakati Ndugu
Wallace Karia alipokuwa Makamu wa Rais wa TFF timu tatu za Tanga Coast
Union, African Sports na Mgambo zilishuka kwa mpigo.
Katika
mfumo wa kitaasisi unaoendesha TFF wenye jukumu la kusimamia Ligi zetu
ni Bodi ya ligi, Ambao ndiyo wasimamizi wa moja kwa moja wa ligi daraja
la kwanza hivyo maamuzi hufanywa kwa kutumia vyombo vya kitaasisi na
hakuna nafasi kwa Rais wa TFF au Makamu wake kuingilia vyombo vya TFF
ambavyo vinafanya kazi ya kusimamia ligi.
TFF
inawajibika kama msimamizi mkuu wa Soka nchini kuhakikisha vyombo vyake
vinatenda haki kikiwemo chombo chake kinachosimamia ligi zetu TPLB.
TFF
pia kwa maelekezo ya Rais Karia kwa Kaimu Katibu Mkuu, ameelekeza
kuangaliwa upya na Kufanyiwa marekebisho ya TIJA kwa Ratiba ya WAAMUZI
(kama itabainika haja ya kufanya hivyo) kwa Michezo yote ya FDL
inayokutanisha TIMU zenye nafasi ya kupanda au kushuka Daraja na
Kuongeza USIMAMIZI katika Michezo hiyo. TFF itakuwa na Vikao vya
Kiutendaji na BODI ya Ligi.
TFF
pia inavitaka Vilabu na Wadau wake wote halali wanaotaka kurekodi
Michezo ya FDL na SDL (ambayo hakuna TV iliyo na HAKI za kuonesha kwa
sasa) kuwasiliana na TFF na Kupata KIBALI kitakacholinda HAKI zao na za
Mchezo (TFF) kabla ya kufanya hivyo. Ni Makosa kurekodi mchezo wowote
kwenye Mashindano ya TFF bila IDHINI ya TFF.
IMETOLEWA NA OFISI YA KAIMU KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA(TFF)
Comments