
Polisi
wamefyetua gesi ya kutoa machozi na kuondosha vizuizi barabarani vya
matairi yalioteketezwa moto kote nchini. kifo hicho kimetokea katika
mji wa kaskazini wa Saba.
Maandamano hayo yalipangwa na wafuasi wa mgombea wa upinzani aliyeshindwa.
Mwezi uliopita, rais aliyepo Juan Orlando Hernandez alitangazwa mshindi licha ya maandamano ya siku kadhaa.
Siku
ya Jumamosi shirika lisilo la serikali mjini Saba, limesema mwanamume
mwenye umri wa miaka 60 aliuawa na mwingine kujeruhiwa wakati polisi
ilipofyetuwa risasi katika kituo cha ukaguzi, shirika la habari la
Reuters, limeripoti.
Uchaguzi huo wa November 25 umeshutumiwa
pakubwa. Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Salvador Nasralla wana shaka
kubwa na tume ya uchaguzi iliyohesabu kura.
Hii ni kwa sababu ilichaguliwa na bunge linalodhibitiwa na chama cha National Party cha Hernández.
Awali Nasralla aliongoza katika kura hizo zilipokuwa zinahesabiwa,
lakini hilo likabadilika haraka na akaushutumu utawala kwa kubadili
matokeo.
Maelfu ya watu waliandamana barabarani katika maandamano ya upinzani kufuatia uchaguzi huo.
Shirika la Amnesty International linasema watu 14 wamefariki katika mapigano, lakini polisi wanasema ni watatu pekee waliouawa.
Rais
Hernández, mwenye umri wa miaka 49, amekuwa madarakani tangu 2013, na
ni rais wa kwanza kuwania muhula wa pili baada ya mahakama ya juu zaidi
ya nchi hiyo kuondosha marufuku ya kuwania muhula wa pili.

CHANZO:BBC.
Comments