
Takriban
wanaume 30 waliojihami kutoka Chad, Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya
kati walikamatwa mwezi uliopita, kulingana na waziri mmoja.
Walipatikana wakiwa roketi, bunduki na risasi kwenye mpaka nchini Cameroon.
Serikali ya Rais Teodoro Obiang Nguema, imekuwa ikilaumiwa kwa ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.
Wanajeshi
nchini Equatorial Guinea walimuua kwa kumpiga risasi mamluki wakati wa
makabiliano siku ya Jumatano karibu na mpaka na Cameroon, kwa mujibu wa
runinga ya taifa TVGE.
Bw. Obiang amekuwa madarakani kwa karibu
miaka 40, baada ya kutwaa madaraka kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi
mwaka 1979 na kumuondoa madarakani mjomba wake Francisco Macias Nguema
ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi.
Katika taarfa iliyosomwa
kupitia radio ya taifa, waziri wa ulinzi Nicholas Obama Nchama
aliwalaumu mamluki waliokuw wamepewa kazi na makundi ya upinzani na
kusaidiwa na mataifa ambayo hayakutajwa.
Alisema kuwa mapinduzi hayo yalizimwa kwa msaada wa idara za usalama za Cameroon.
Equatorial Guinea imekumbwa na madai ya mapinduzi ya kijeshi siku za awali.
Mwaka 2004 mwanajeshi wa zamani raia wa Uingereza Simon Mann alihusishwa na jaribio la kumpindua Obiang.
Mwanajeshi
huyo wa zamani wa Uingereza na mafanyabiashara alikamatwa nchini
Zimbabwe mwaka 2004 na kusafishwa kwenda Equatorial Guinea miaka minne
baadaye.
Mwaka 2008 Bw. Mann alihukumiwa miaka 34 jela, lakini mwaka mmoja baadaye aliachuliwa baada ya kusamehewa na Bw. Obiang.
Equatorial
Guinea ni moja ya nchi wazalishaji wakubwa wa mafuta lakini asilimia
kubwa ya watu wake wanaishi katika hali ya umaskini.
chanzo:Bbc..
Comments