
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Dk Kahangwa alipendekezwa na
NCCR-Mageuzi kuwania urais ndani ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) ili kupitishwa kupeperusha bendera ya umoja huo.
Dk Kahangwa ambaye ni msomi wa masuala ya elimu ametangaza uamuzi huo
kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Facebook ikiwa ni kipindi ambacho
kumekuwa na wimbi la wanasiasa wa upinzani kuhamia Chama cha Mapinduzi
(CCM).
“Mniwie radhi kuwataarifu hili. Sioni dalili yoyote ya mwanga
katika chumba cha giza nene linaloigubika NCCR- Mageuzi. Hivyo, hiari
ileile niliyoitumia kujiunga, sasa naitumia kukaa pembeni,” amesema Dk Kahangwa katika ujumbe aliouweka Facebook.
Mkuu wa Oganaizesheni na Utawala wa NCCR-Mageuzi, Florian Mbeo amethibitisha kujiondoa kwa Dk Kahangwa.
“Ni kweli amejivua uanachama, alikieleza chama kuhusu suala
hilo na hata leo asubuhi nimezungumza naye. Uamuzi aliochukua ni wa
kawaida tunauheshimu,” amesema Mbeo.
Akitoa maoni kuhusu ujumbe wa Dk Kahangwa Facebook, Mathias Mbeho amesema, ‘’Mkuu
kwa kweli huko ulipotea gizani. Kwa wewe ulivyo unatakiwa kumuunga
mkono ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika Taifa hili.
Nayaona maisha yako mapya na mazuri kwenye ulingo wa siasa. Wise
decision.”
Abdul Migeyo Juma amesema, ‘’Nakupongeza kwa kufanya maamuzi
Dr Ila sababu yako siyo ya kisomi hata kidogo, unadhani mwanga unaletwa
na nani? asee hapa ndio nashindwa kuelewa ukombozi wa kifikra juu ya
elimu tuipatayo Watanzania, Nadhani tutafika hatua ya kutowapeleka
watoto shule maana matokeo ya wasomi wetu kwenye jamii yakiwa hivi
mnatutia wasiwasi juu ya kusomesha watoto!! Au elimu yetu ndio
inatufanya tuwe hivi? Kipindi hiki kilikuwa si sahihi kwako kutoka NCCR
hata kama ni haki yako.”
chanzo:Zanzibar24.
Comments