
Mchezaji
mpya aliyesajiliwa kwa pauni milioni 15 kutoka Everton Ross Barkley
hatoshiriki kwa kuwa bado anauguza jereha la nyuma ya goti.
Mkufunzi
wa Arsenal Arsene Wenger ataendelea na marufuku ya kutokalia eneo la
wakufunzi uwanjani na badala yake kukaa katika viti vya mashabiki huku
kikosi chake kikirudi baada ya kufungwa na klabu ya Nottinham Forest
katika kombe la FA.
Granit Xhaka anauguza jeraha la kinena huku Shkodran Mustafi ambaye aligongwa akiwa hajulikani iwapo atashiriki.
Mfumo wa kiteknolojia wa video ya kumsaidia refa VAR utatumika katika awamu zote mbili za nusu fainali hiyo.
Arsenal haijashinda kombe hilo kwa kipindi cha miaka 25 huku Chelsea ikiweza kushinda mara ya mwisho 2015.
chanzo:Bbc.
Comments