Naibu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum
ametangaza vita na chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Ubunge jimbo la
Kinondoni.
Akizungumza
baada ya kuchukua fomu Mwalimu amewataka wanachama wa chama hicho kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki cha muda mfupi.
Kwa hiyo baada ya muda huo kupita
siku ya kesho bila ya shaka nitakuwa mgombea rasmi wa jimbo la Kinondoni ambaye
nisiyekuwa na doa kwa ajili ya mapambano hayo alisistiza Mhe. Salum
Mwalimu.
|
Mwalimu amesisitiza kuwa safari
hii hawakuja kubip katika kinyang’anyiro cha Ubunge Kinondoni kama
ilivyojitokeza katika chaguzi nyingine za marudio zilizopita.
|
Tunamaanisha na tunaamini kabisa
kama nidhamu ya siasa waliyoikataa, hapa watairudisha na wasipoikubali
kuirudisha Kinondoni maana yake ustaarabu katika siasa tunaamini utakuwa
umekwishamalizika. Hatutokuwa wa kulia, safarii hii ikibidi tutawasababisha wale
waliosababisha sisi tunalialia wao ndio walie
|
Amesema Mwalimu Kuhusu dhamira yake ya kugombea
Ubunge, Mwalimu amesema amedhamilia na amejitoa kusimamia haki ya wananchi wa
Jimbo la Kinondoni na kuahidi hatoweza kuyumba
|
Comments