Baraza la manispaa lajipanga kuung’arisha mji wa Zanzibar.

Baraza la Manispaa Zanzibar litahakikisha  sheria zilizopangwa zinatekelezwa  kwa  mikakati  madhubuti kwa lengo la kuuweka mji wa Zanzibar katika mazingira bora na salama kwa raia.

Akizungumza na Zanzibar24 Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar Aboud Hassan Serenge amesema kwa mwaka 2018  watahakikisha  sheria zote  zilizopangwa kuimarisha mazingira kwa upandaji wa bustani pamoja na udhibiti wa taka zinafanikiwa ili kulinda mandhari ya nchi.

Serenge amesema  mashirikiana  baina ya serikali wananchi na baraza hilo yanahitajika ili kufanikisha adhma ya kuufanya mji wa Zanzibar kuwa na haiba nzuri hali itakayosaidia kupunguza maradhi yanayoambukiza ikiwemo kipindupindu.

chanzo:Zanzibar24

Comments