Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi Azam FC watakuwa
kwenye mtihani mgumu kuhakikisha wanashinda mechi yao ya Kundi A ili
kufuzu kucheza nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea visiwani
Zanzibar, Azam wamepoteza mchezo wao wa tatu dhidi ya URA kwa kufungwa
goli 1-0.
Azam ipo katika nafasi ya pili hadi sasa kwenye Kundi A ikiwa na
pointi sita nyuma ya URA ambayo ina pointi saba baada ya kucheza mechi
tatu. Endapo Azam itapoteza mchezo wake dhidi ya Simba, moja kwa moja
itajikuta nje ya mashindano hayo kwa sababu Simba itafikisha pointi saba
huku ikiwa na mechi moja mkononi wakati Azam watakuwa wamemaliza mechi
zao za hatua ya makundi.
Azam imeshacheza mechi tatu hadi sasa, imeshinda mechi mbili (Mwenge
1-2 Azam, Jamhuri 0-4 Azam ) huku wakipoteza mchezo mmoja (Azam 0 -1
URA).
Kundi A lina timu tano URA (Uganda), Simba, Azam (Tanzania bara),
Jamhuri na Mwenge (Zanzibar). Mechi ya Azam vs Simba itachezwa Jumamosi
January 6, 2018.
Comments