
Almasi hiyo iliyo patikana katika mgodi mdogo wa Lesotho, Afrika Kusini ni nusu ya ukubwa wa moyo wa kiume wa binadamu.
Kutokana na Gazeti la “New York Times” inaripoti
kwamba kampuni ya Diamond Gems iligundua Almasi hiyo katika mgodi wa
Letseng iliyopo Afrika Kusini na inasemekana kwamba Almasi hiyo haina
rangi wala uchafu wowote ambao ungepunguza ukubwa wake.
Serikali ya Lesotho inamiliki sehemu ndogo katika mgodi wa Letseng ambayo inamilikiwa na wadau wengi kutoka British.
Almasi hiyo ndiyo Almasi kubwa zaidi kupatikana katika Leostho nchi
ndogo iliyozungukwa na Afrika Kusini. Jiwe ambalo liliweka heshima hadi
leo ni Lesotho Promise ambalo lilikuwa na karamu 603 na kuuzwa kwa kiasi
cha dola milioni 12.4 kwa mnada zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Kwa taarifa zilizotolewa leo ni kwamba Gavana Mkuu wa Gem Clifford Elphick alisema jiwe la hivi karibuni lililogunduliwa ni “exceptional top quality diamond” yaani almasi yenye ubora waki pekee yenye kiwango cha juu zaidi cha rangi.
chanzo: zanzibar24.
Comments