Tayari kuna timu kadhaa za Afrika Kusini na Morocco zimeonyesha nia ya kumtwaa mshambulizi, Habibu Kiyombo wa Mbao FC.
Hii inatokana na mabao yake matatu aliyofunga katika mechi za Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga na Simba.
Tayari
mmoja wa mawakala walio fasta ametuma video za mabao hayo matatu na
anasema, inaonekana wamevutiwa ingawa kuna ugumu wa kutoa fedha.
“Nimetuma
video zake, unajua nilianza kumfutilia baada ya kuifunga Simba bao zuri
sana walipotoka 2-2. Lakini nimeona amerudia kufunga bao lenye ubora
uleule.
“Kazi
yangu ni kuhakikisha Tanzania ina wachezaji wengi wa kulipwa na
nimekuwa nikifanya hivyo kwa kuwafuatilia wachezaji wengi,” alisema
wakala huyo ambaye kaishawapeleka wachezaji kadhaa maarufu wa Tanzania
na wengine wanacheza nje.
“Kama
wataridhika naye na watakuwa na ofa nzuri, basi moja kwa moja nitaanza
kuwasiliana na Mbao FC ili kumpa nafasi ya kwenda nje,” alisema.
Hata hivyo, wakala huyo hakutaka kuandikwa akidai angependa kufanya mambo yake kimyakimya hadi yatakapofikia wakati sahihi..
Comments