
Akizungumza Kwa Niaba ya Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali katika semina ya siku mmoja kwa Wajumbe hao ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika taasisi hiyo,
Prof. Ali Seif Mshimba amesema iwapo wawakilishi watawasilisha michango yao binafsi itasaidia kuimarisha miundombinu iliyopo kutokana na taasisi kukabiliwa na tatizo la uhaba wa miundombinu ya kisasa.
Amesema wanashindwa kufikia malengo waliyokusudia ya kuhakikisha bidhaa zote zinachunguzwa ubora wake kwa wakati husika kabla ya kutumiwa na wananchi kutokana na kutokuwa na Majengo na Vifaa vya kisasa vya Maabara Vinavyoendana na Ukuwaji wa Teknolojia.
Aidha amesema mpaka sasa Taasisi hiyo ina maabara mbili Ikiwemo Maabara ya Umeme na kemikali kwa ajili ya kupimia ubora wa mafuta ya nishati jambo ambalo linawalazimu bidhaa nyengine kupelekwa kuchunguzwa kwa mkemia mkuu wa serikali wa Zanzibar na bidhaa nyengine kupelekwa kupimwa TBS Tanzania Bara.
Amesema katika kuhakikisha Bidhaa zinazotumika hazileti athari kwa watumiaji mpaka sasa jumla ya sampuli 115 za bidhaa mbalimbali zimechukuliwa na kupelekwa maabara Septemba 2017,ambapo bidhaa kumi na nane zimeonekana zipo chini ya kiwango na teari zimechukuliwa hatua za kisheria ili kulinda afya ya mlaji na Mtumiaji.
Nae Mkurugenzi wa ZBS Khatib Mwadini amesema Semina hiyo itasaidia kujenga ueledi juu ya Umuhimu wa matumizi Bora ya bidhaa zenye viwango katika jamii ili kujenga misingi ya uchumi na ustawi wa jamii Nchini pamoja na kulinda Afya za walaji na Mtumiaji wa Bidhaa hizo.
Kwa upande wao Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Waliishauri Taasisi ya Viwango Zanzibar ZBS kufanya kazi kwa kufuata sheria pamoja na kujenga utamaduni wa kuazisha Elimu ya viwango maskulini ili kuwajengea uwezo wanafunzi kujua umuhimu wa kutumia bidhaa zenye viwango.
Hata hivyo amesema ZBS watakapojikita na Utaji wa Elimu ya Viwango na Ubora wa Bidhaa katika Maskuli itaisadia Selikali kuwa na wataalumu wa Uhakika watakaosimamia masuala ya viwango katika taasisi hizo jambo ambalo litachangia kuimarisha Uchumi wa Nchini.
Semina hiyo ya siku Moja Iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar imeshirikisha kamati tatu ikiwemo kamati ya Ustawi wa jamii ,Kamati ya fedha,biashara na Kilimo pamoja na Kamati ya Bajeti ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya Umuhimu wa bidhaa zenye viwango.
chanzo: Zanzibar24.
Comments