Kwa mujibu wa Chama cha Wafungwa Wapalestina, kwa akali Wapalestina
610 wametiwa nguvuni wakiwemo watoto wadogo 170 na wanawake 12.
Ripoti ya taasisi hiyo imenukuu takwimu za Umoja wa Mataifa
zinazosema kuwa, kati ya Disemba 5 na 18, vikosi vya usalama vya Israel
vimefanya operesheni za upekuzi na kamatakamata 162 katika ardhi za
Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Licha ya kamatakamata hizo, lakini viongozi na shakhsia mbali
mbali wa kisiasa wa Palestina wametangaza kuwa Intifadha ya Wapalestina
itaendelea hadi utakapofutwa uamuzi uliotangazwa na Rais wa Marekani wa
kuitambua Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni.
Itakumbukwa kuwa tarehe 6 Disemba, Trump aliamsha hasira za
Wapalestina na walimwengu kwa ujumla, kwa kutangaza kuitambua Baitul
Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel na kuagiza
zichukuliwe hatua za maandalizi ya kuuhamishia katika mji huo ubalozi wa
Marekani ulioko Tel Aviv.
Comments