Dereva mmoja wa basi la mwendokasi la Kampuni ya Gold Coast nchini Australia amesimamishwa kazi baada ya video yake kuvuja ikimuosha akijisaidia haja ndogo mlangoni mwa basi hilo.
Kamera hizo zilimnasa dereva huyo akiwa mlangoni akijisadia haja ndogo bila kujua kama anarekodiwa na baadaye kuingia ndani ya gari ambalo ndani kulikuwa na abiria wawili pekee.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ndiye alirekodi tukio video hiyo ameeleza kuwa alifanya hivyo kama makusudi baada ya wiki kadhaa kampuni hiyo kulaumiwa na wateja kuwa madereva wa kampuni hiyo hawana nidhamu.
“Tumeiona video hiyo na muhusika tumesha msimamisha kazi kwa ajili ya kupisha uchunguzi, Tunajua matukio haya ni mabaya kwenye jamii na kwa kampuni yetu hivyo kama itakuwa ni kweli muhusika tutamchukulia hatua za kinidhamu zaidi.“ameeleza msemaji mkuu wa Kampuni ya Gold Coast.
chanzo:zanzibar24.
Comments