Tasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza
utaratibu wa familia za kabila la Kichaga kutumia majani maarufu kama
‘sale’ kufunika au kumaliza kienyeji kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia
na mimba za wanafunzi.
Majani
hayo ya masale kwa mila na tamaduni za kabila la Wachaga, hutumika
kuashiria amani, kuomba msamaha na kumaliza tofauti zao.
Ofisa
wa Takukuru Wilaya ya Hai, Denis Mazigo, amefichua siri hiyo ya kuanza
kwa uchunguzi dhidi ya mila hiyo wakati wa uwasilishaji ripoti ya kamati
ya ulinzi wa mtoto.
“Haliwezi
kutangulizwa jani la sale peke yake, lazima kuna mazingira ya kutolewa
kwa fedha kama rushwa, ndiyo msamaha uweze kukubalika. Sasa sisi kama
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa tumeanza kufanyia kazi jambo
hili, kwa sababu tumeona kesi nyingi za ukatili zikikwama huku zikiwa na
ushahidi wa kutosha,” alisema Mazigo.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments