
Kwa sasa naishi Mbagala, jijini Dar es Salaam na familia yangu yenye
mke na watoto saba, wote wa kike. Mke wangu pia kwao ni mtoto wa kwanza
katika familia yenye watoto tisa, wote wanawake.
Nimelazimika kusimulia mkasa huu wa kichawi baada ya watu wengi
kusimulia mikasa yao wakidai waliwahi kuwa wachawi wakaacha kwa sababu
mbalimbali ambazo wengine huzisema, wengine hufanya siri kubwa.
Naweza kusema kwamba, karibu wote waliokuwa wakisimulia maisha yao ya kichawi na mikasa yake, hakuna hata mmoja aliyewahi kufikia hata robo ya maisha ya kichawi ya kwangu.
Mimi niliishi maisha hayo kwa miaka kumi, na nilifika ‘levo’ ya
mbali, mfano kuwa Mkuu wa Kikundi na kusafiri sehemu mbalimbali duniani
kwa ajili ya mikutano mikubwa ya kimataifa ya wachawi na niliporudi,
nilikuwa nakutana na wachawi wakubwa wa hapa nyumbani Tanzania na kuwapa
maagizo ya utendaji katika makundi yao sehemu mbalimbali za nchi.
Katika kipindi chote cha kuwa mchawi nilibaini mambo makubwa mawili,
kwamba, maisha ya wachawi katika ulimwengu wao hayana tofauti yoyote na
maisha ya watu wasio wachawi katika ulimwengu huu wa macho ya kawaida.
Maandiko yanaposema kuwa, Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na
visivyoonekana ni kweli kabisa. Wachawi wanaamini kwamba, vitu
visivyoonekana pia vilikuwa na siku sita katika uumbaji wa Mungu, siku
ya saba akapumzika. Na hiyo ndiyo sera ya mchawi mara tu baada ya
kujiunga katika kazi hiyo inayolaaniwa na wengi ulimwenguni kote.
Kabla sijaenda mbele zaidi nataka kusema kuwa, kama kuna shughuli
mbalimbali za binadamu zinazoonekana kwa macho ya kawaida duniani, pia
kuna shughuli kama hizo hizo zisizoonekana kwa
Wachawi wana kila kitu, wana mikutano ya nchi, mikutano ya kimataifa,
ya kanda ya mabara na pia wana mabenki, japokuwa kwa macho
tunazungumzia mabenki ya pesa, wao wana mabenki ya damu, nyama na dawa
za kienyeji.
Itaendeleea………………………………………….
Hadithi hii imeandaliwa na kuletwa kwenu na mbdully.wordpress.
Comments