Mhe Haruon
ameyasema hayo leo huko katika viwanja
vya Hospital ya Abdullah Mzee Mkoani
ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho kutimia miaka 54 ya Mapinduzi
matukufu ya zanzibar zilizoanza leo.
Amesema sera za
Mapinduzi ya mwaka 1964 imeahidi
bayana kuwapatia wananchi wake huduma
muhimu za ayfa bila ya malipo ,jambo
ambalo linaendelezwa hadi sasa.
Mapema Mhe Haroun amewasisitiza wananchi kudumisha
suala la usafi hususan katika maeneo ya mahospital ,ili kulinda ayfa za wananchi.
Amesema suala la
usafi ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu,hivyo ni vyema jambo hilo kuendelezwa.
Naye Kaimu Mkuu
wa wa wilaya ya Mkoani ,ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya chake chake Ndg Rashid
Hadidi Rashid amesema kuwa wilaya hiyo
imejipanga vyakutosha kusimamia suala la
usafi katika maeneo mbali mbali wilayani humo ikiwa ni pamoja nakutoa mafunzo
kwa wananchi juu ya udhibiti na usimamizi mzuri wa mazingira.
Comments