
Akizungumza na wanahabari katika mazungumzo yenye nia ya kubadilishana mawazo, hafla iliyofanyika leo katika Hoteli ya Zanzibar Ocean view, Kilimani Mjini Unguja.
Mhe. Raza amesema kwa sasa hali ya ukusanyaji wa kodi na mapato mengine kwa serikali zote mbili imeimarika tofauti na ilivyokuwa awali hali inayochochea kasi ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Pamoja na hayo amewasihi wafanyabiashara nchini kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima baina yao na Serikali.
Mapema asubuhi Mhe. Raza aliungana na wanahabari katika maandamano ya amani kuwaenzi wanahabari ambao kupitia kazi zao wamekuwa chachu ya kuleta maendeleo nchini.
Maandamano hayo yalianzia Baraza la zamani la wawakilishi Kikwajuni mjini Unguja hadi katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
chanzo:zanzibar24.
Comments