
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issa, amesema kwamba
mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Karanga katika Halmashauri ya
Manisapaa ya Moshi, alikamatwa akiwa na kilogramu 216.3 za bangi ndani
ya gari lake aina ya Toyota Sienta.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa eneo la Majengo kwa Mtei, Disemba 19 alipokuwa njiani akitokea Himo.
Kamanda Issa amesema kuwa, biashara ya bangi inabaki kuwa changamoto
kubwa sana katika mikoa ya kaskazini, na kwamba jeshi la polisi
linafanyakazi kwa jitihada zote kuhakikisha linatokomeza hali hiyo.
Aidha, alionesha masikitiko yake kufuatia watumishi wa umma ambao
ndio walitakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita dawa za kulevya,
wakijihusisha kwenye biashara hiyo.
chanzo: zanzibar24.
Comments