
Mti huo unaofahamika kama "Jackson" magnolia ulipandwa na rais Andrew Jackson kama kumbukumbu kwa mke wake.
Umekuwa
ukionekana kwa picha wakati wa sherehe nyingi huko White House na hata
picha zake ziliwekwa kwenye noti za dola 20 kati ya mwaka 1928 na 1988.
Lakini
wataalamu wanasema kuwa mti huo umeharibiwa na kuwa hatari kwa usalama.
Mke wa Trump Melania Trump ametaka sehemu kubwa ya mti huo kukatwa.
Msemaji wa White House Stephanie Grisham anasema Bi Trump alichukua
hataua hiyo kwa sababu mti huo ulikuwa ni tisho kwa usalama wa wageni na
waandishi wa habari ambao mara nyingi husimama mbele yake wakati
helikopta ya rais inapaa.
Mtu wa Magnolia ulipandwa kutoka ya mti wa magnoalia uliokuwa ukipendwa na Rachel Jackson katika shamba lao huko Tennessee.
Marais
39 wamehudumu mti huo ukiwa White House na pia ulikuwepo wakati wa vita
vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani na vita vya kwanza na vya pili
vya dunia.

chanzo:bbc.
Comments