
Wizara
ya fedha nchini Marekani iliwataja Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol na
kusema kwua wote walikuwa viongozi wakuu katika mpango wa makombora ya
masafa marefu wa Korea Kaskazini.
Baraza la ulianzi la Umoja wa Mataifa liliiwekea vikwazo vipya
Korea Kaskazini siku ya Ijumaa kujibu majaribio yake ya makombora ya
masafa marefu.
Korea Kaskazini ilisema kwa hatua hiyo ni kama ya vita.
Vikwazo hivyo vipya vya Marekani vitazuia shughuli zozote za wanaume
hao wawili zinazofanywa nchini Marekani, na hata kutwaliwa kwa mali yao
yaliyo nchini Marekani.
Wanaume hao wawili wanaonekana mara kwa
mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakiwa maeneo ya
kuyafanyia majaribio makombora.
Mwaka huu nchi hiyo imefanya majaribio kadha ya makombora tofauti ambayo nasema kuwa yanaweza kufika nchini Marekani.

Comments