Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka na kutoa utabiri wake wa
majibu ambayo Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship
(FGBF), Askofu Zakaria Kakobe atawapa Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhusu
mali na utajiri wake.
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) jana ilisema kuwa inataka kufanya uchunguzi mali za
Askofu huyo ili kujua chanzo halisi cha utajiri wake kufuatia Askofu
huyo kudai kuwa ana fedha kuliko Serikali.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments